Page 109 - Your Guide to University Life
P. 109
-Weka jitihada na nguvu kwenye masomo ili upate matokeo mazuri na hata ukipata ambayo sio mazuri hautojilaumu kwasababu unajua uliweka jitihada zako zote.
-Kwenye jambo lolote usijihukumu sana, uwe mkarimu kwako mwenyewe kwanza, ifundishe ile sauti akilini mwako kusema maneno makarimu nay a upole kwako. Mara nyingi huwa tunajiambia maneno makali sana ambayo hauwezi kumuambia mtu mwingine kwa jinsi yanavyoumiza, jitahidi kupunguza kujiambia maneno yanayoumiza sana katika hali yoyote ile.
-Usiwe na vitu vingi vya kuviwaza au kuvifanya. Jua jinsi ya kutuliza hisia zako, jua hisia gani unayo na unaitulizaje katika njia ambayo haina madhara kwako
-Toka nje
Jua na uota wa asili husaidia sana mwili na akili kupumzika.
-Usitumie sana vilevi na madawa (au usitumie kabisa).
-Jijengee tabia ya kucheki afya yako ya akili pia kama vile unavyoenda hospitali kucheki afya ya mwili.
Jiulize; Unajisikiaje? Inasababishwa na nini hiyo hisia? Na unaweza kufanya nini ili kusuluhisha hilo?
109