Page 107 - Your Guide to University Life
P. 107
-Kupitia presha au woga wa mtihani nk -Kupitia matatizo nyumbani ya kifamilia -Changamoto za ujana nk
Afya yako ya akili inaweza kuathiriwa na mambo mbalimbali ila kuna tabia ambazo unaweza kuwa nazo zinazoweza kukusaidia uwe katika hali nzuri ya afya ya akili kama kijana na mwanachuo, na tabia hizo ni kama vile;
-Kufanya mazoezi
Mazoezi ni njia nzuri ya kuchangamsha mwili na kuondoa stress za mwili. Relax na fanya mazoezi ya kupumua.
-Kuwa na mapumziko ya mitandao ya kijamii
Kama vijana tunatumia muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii, na wengi wetu tunajilinganisha na wale tunaowaona na kujisikia kama vile maisha yetu sio mazuri ukilinganisha na ya wale tunaowaona mitandaoni. Ukichukua mapumziko ya mitandao unaweza kufocus zaidi kwenye masomo lakini pia unaweza kuona kuwa maisha ni zaidi ya yale unayoyaona tu mtandaoni.
-Kupumzika
Kwa kulala (lala vizuri na kwa wakati) au kwenda sehemu nyingine mbali na chuo siku za mapumziko. Hili linaweza kufanya akili yako isiwe inawaza jambo hilo hilo moja linalokupa msongo wa mawazo.
107