Page 106 - Your Guide to University Life
P. 106

Jinsi ya kujali afya yako ya akili unapokuwa chuo
Kutokana na stress mbalimbali chuoni, zikiwemo za masomo, mahusiano, familia, uchumi, marafiki na shida tu za ujana, unaweza kuta afya yako ya akili inakuwa haiko vizuri uwapo chuoni.
Kutokana na mazingira ya chuo na maisha ya chuo yalivyo, haya hapa ni mojawapo ya magonjwa ya akili yanayowakumba sana wanachuo;
1. Sonona / Depression
2. Wasiwasi / Anxiety
3. Matatizo ya kula / Eating disorders
4. Ulevi wa madawa / Drug abuse
5. Utegemezi wa kilevi / Alcohol abuse nk
Kuna vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia kuathirika kwa afya yako ya akili chuoni, vitu hivyo ni kama vile;
-Kuachana na mpenzi wako / matatizo ya mahusiano na watu mfano roommates au classmates / kufiwa na mtu wa karibu au unayemfahamu / kumpoteza mtu wa karibu yako mfano urafiki kuvunjika nk
-Kutotimiza matarajio yako kwenye matokeo -Kukosa pesa / kupitia changamoto -Upweke
-Kubakwa
-Ugonjwa wa muda mrefu
 106





















































































   104   105   106   107   108