Page 105 - Your Guide to University Life
P. 105

-Kunywa maji, mengi na ya kutosha. Asilimia kubwa ya miili yetu ni maji.
-Balance muda wako wakuangalia filamu, sio vizuri sana kwa afya ya macho yako kila saa kuwa kwenye mwanga na kioo cha laptop unaangalia muvi. Nilipoingia chuo nilikuwa naona vizuri hadi mbali lakini baada ya mikesha ya muvi na kila kitu, sasa sioni mbali. Usiwe kama mimi uwe na kiasi, kula karoti na pumzisha macho yako muda mwingine.
- Jali afya yako ya meno. Meno yako yasafishe, usile nyama sana and vyakula vyenye sukari sana. Nakuambia hivi kwa vile mimi baada ya chuo ilibidi nikazibe meno kwasababu nilikuwa nakula nyama kwenye kila mlo na meno yakasumbua ikabidi nizibe.
-Pia usafi wako wa mwili, na kufua nguo, weka muda kwa ajili ya hayo, jipende.
-Nenda hospitali ya chuo muda unaohisi hauko sawa, ujue mwili wako vizuri kujua pale ambapo hauko sawa kihisia na kimwili. Au pia panga muda wa kuwa unaenda kucheki afya, kwa vile una kadi ya afya ya chuo itumie ipasavyo.
Usijipuuzie, usiupuuzie mwili wako, kuupuzia mwili wako ni kutokujipenda. Jioneshe upendo wewe kwanza.
105




























































































   103   104   105   106   107