Page 104 - Your Guide to University Life
P. 104

Hizi hapa ni njia chache unazoweza kuzitumia kujali afya yako ya mwili:
-Usipige pasi ndefu labda kama umefunga, hata kama umebanwa sana na ratiba siku hiyo, jitahidi basi ule hata mkate.
-Jitahidi kula mlo kamili, kula matunda, kunywa maji nk. Vyakula hivi vinaweza visiwe na gharama kama mchana unakula hiki na jioni unabadilisha unakula kile.
Lakini pia muda mwingine kama unapenda kupunguza gharama za vyakula basi jaribu kuweka bili.
-Fanya mazoezi, hii inafaa pia hata kwaajili ya akili, mazoezi yanasisimua ubongo pia hata katika kufikiri. Ukitenga hata lisaa limoja kwaajili ya gym au hata kukimbia au kujiunga timu ya mpira wa miguu au kikapu, basi itakuwa poa zaidi kwa afya yako. Fanya jogging asubuhi au jioni, piga push ups na squarts, planks na mazoezi ya kukuweka fit kuepuka accumulation ya fats na magonjwa nyemelezi yaani kiufupi yafanye mazoezi kama sehemu ya maisha yako ukiwa chuo na hata baada ya kutoka. Vyuo vingi huwa na gym za karibu au ndani ya chuo ambazo malipo yake yako chini zaidi hasa kwa wanachuo, hivyo unaweza chukua advantage ya hili. Gym husaidia sana, zaidi ya mazoezi ya mwili inasaidia mtu awe na nidhamu ya wakati na pia kuwa mwangalifu wa kile unachokula, mambo ambayo yatakusaidia sana kujiendeleza.
104





























































































   102   103   104   105   106