Page 103 - Your Guide to University Life
P. 103

Afya yako chuoni
Ukiwa chuo vitu vya muhimu vya kuvijali ni masomo yako na afya yako, afya yako ya mwili na ya akili. Afya yako ni ya muhimu kuijali na kuiangalia kwa jicho la karibu kwasababu ukiwa hauna afya nzuri, yani mgonjwa unakuwa hauwezi kusoma mpaka upate matitabu. Na ukiwa unasoma sana bila kujali afya yako kwa kupumzika na kula vizuri pia utaifanya afya yako iathirike na madhara ambayo yanaweza kuwepo kwa muda mrefu hata baada ya chuo mfano kupata vidonda vya tumbo nk.
Kipindi uwapo chuo ni kipindi ambacho unajitegemea mwenyewe kwenye uamuzi wa nini ule nk, na ujio wa wajibu huu unaweza kukufanya ukashawishika kutokula mlo kamili na kuishia tu kula chipsi mchana na usiku kama mimi nilivyofanya na kuishia kutokujali afya yako. Mfano mimi, nilikuwa nakula chipsi kila siku kuanzia mwaka wa kwanza mpaka watatu, mchana na jioni, nikibadilisha ni siku moja moja, kwasababu niliamini niko mbali na nyumbani na nina boom, basi sasa niko huru kula chakula changu pendwa, jambo ambalo ni kweli lakini haimaanishi nisijali afya yangu na kutokula mlo kamili au kufanya mazoezi.
Chuoni jitahidi kujali afya yako, ya akili, ya mwili, nafsi na roho. Afya yako ndio sababu kuu unaamka asubuhi na kwenda darasani, ukiumwa hauwezi tena kufanya jambo hili linalokufanya uwe mwanachuo. Hivyo kuwa makini sana na jali afya yako.
 103






























































































   101   102   103   104   105