Page 101 - Your Guide to University Life
P. 101

kama ni boom tu na presha za kikundi chako ndio zinakufanya uwe hivyo ulivyo.
Ikiwa kuna mtu basi akakushuhudia ukiwa unaishi maisha fake au unaigiza ya watu basi yeye atasema kuwa umebadilika, lakini pia unaweza badilika kwa kuishi staili mpya ya maisha unayoichagua ambayo hapo kabla haukuwa nayo mfano unaweza fika chuo na ukapenda kwenda club inaweza isiwe umemgeza mtu au unaigiza maisha ya mtu ila mtu akasema umebadilika kwasababu hapo kabla alivyokuwa anakufahamu haukuwa mtu wa club.
Watu wengi hubadilika chuoni kutokana na uhuru, kutokana na kuwa na pesa za kuweza kulipia gharama za hayo maisha wanayoyatamani lakini pia kutokana na ukuaji na hivyo mtu unaamua kuchagua maisha fulani ya kuyaishi kwa chuo mara nyingi unaangalia yanayokubalika au yanayoonekana yanafaa mbele za watu chuoni kwa wakati huo.
Wanasema ukifika chuo unakuwa huru, ni kweli, ila pia uhuru unawapumbaza sana watu. Uhuru wa chuo unakuja hivi; ratiba zote kasoro za darasani unajipangia, tofauti na ukiwa nyumbani ambapo unakuta familia inakupangia sana, chuo inaonekana ni kipindi cha uhuru na kujitegemea kwa vile unapesa (kama umepata boom) lakini pia unajipangia jinsi ya kutumia muda wako unaobakia.
Usijaribu ku-fit in sana kwenye vibe la chuo au kwenye vikundi unavyoviona wewe ndo vinatrend nk mpaka ukajibadilisha kabisa vile wewe ulivyo na uhalisia wako kiasi kwamba mpaka wewe mwenyewe ukawa haujijui wewe ni nani.
101





























































































   99   100   101   102   103