Page 100 - Your Guide to University Life
P. 100
Kuigiza maisha / ku-fake maisha / kwanini watu wengi wakifika chuo hubadilika?
Ni vizuri kuchukua mambo mazuri kutoka kwa watu unayoyaona yanakuvutia, mfano tabia nzuri zao unazoona zinaweza kukusaidia kwenye maendeleo yako binafsi.
Kuigiza maisha ni tofauti na huku, kuigiza maisha ni kuchukua tabia yoyote tu kutoka kwa watu bila kufikiria jinsi gani inaweza kukuathiri au muda mwingine kufanya mambo yanayofanana na wanayoyafanya wao kwa vile unahisi vitakufanya uwe kama wao / upendwe kama wao / au uonekane uko ‘up to date / cool’.
Sio rahisi kuelezea sababu za kwanini watu huigiza maisha ya watu wengine, ila inaweza kuwa kwa vile wanaona ya kwao hayavutii / hayapo – cool ukilinganisha na ya wale wanaowaigiza, au wanaona aibu kuishi maisha yao halisi au wanatamani kukubaliwa na watu fulani, kuonekana ni mtu wa aina fulani au kundi fulani linalopendwa. Hizi pia zinaweza kuwa sababu za watu kuishi maisha fake, nyumbani ni watu wengine na vyuoni wanaishi maisha mengine.
Na chuoni ni sehemu rahisi ya watu kuigiza au ku-fake maisha kwa kuwa ni sehemu ambayo wengi ndio tumekua na kuanza kujitambua na kuwa na misimamo binafsi, hivyo muda huo unakuwa bado unaendeshwa / unashawishika na presha kutoka kwa marafiki ‘peer pressure’ na tamaa za ujana lakini pia chuoni hakuna anayejua maisha yako halisi au wachache wanayajua kwahiyo hivyo unavyoishi watu wa chuo wanaokuona watahisi ndio maisha yako halisi hata
100