Page 98 - Your Guide to University Life
P. 98

Vitu vya kufanya unapokutana na skendo:
- Tafuta mtu au watu unaowaamini wa kuwa karibu na wewe kipindi hicho
- Usidhani kuwa huo ni mwisho wa dunia, mambo hayo huwa yanapita baada ya muda
- Tafuta namna ya kudili na aibu na kuchekwa na jamii, jua kuwa kuna watu watakutenga, waliokuwa marafiki zako watakusema nyuma yako, jua kuwa utachekwa lakini ni kwa muda tu au muda mwingine hiyo skendo inaweza dumu muda mrefu zaidi kwa sababu ya mambo haya ya mitandao ya kijamii na teknolojia.
Jua kuwa watu watasahau lakini pia jiandae kwenye mazingira ya huko mbeleni ambayo unaweza kutana na watu ambao hawajasahau au wakakucheka tena kuhusu hilo, mitandaoni au kwenye maisha ya kawaida
- Ongea hata na mshauri nasaha
- Jali sana maoni ya watu wachache unaowathamini lakini pia kuwa karibu sana na watu wanaokutia moyo na kukuambia maneno chanya
- Jisamehe na msamehe huyo aliyekufanyia hivyo. Kama utaamua kumfungulia kesi mahakamani pia kuna sheria katika hili.
 98


























































































   96   97   98   99   100