Page 96 - Your Guide to University Life
P. 96

mwanzoni hayatokubana sana, mfano ukaingia kwenye siasa huko mbeleni au uongozi wowote, mambo uliyokuwa unafanya kwanza yasikuzuie au kukufanya uonekane haustahili.
Ila pia jitahidi kutokuweka mambo yako mtandaoni, tofauti ya kizazi hiki na kile kilichopita ni kuwa; kizazi kilichopita kilikosea ila kulikuwa hakuna camera na mitandao ya kijamii ambapo watu wanaenda kuona mambo ambayo wao wame-tweet au wameweka Instagram. Kizazi hiki tunajibania wenyewe na kufanya tuhukumiwe na watu kirahisi kwa kuwa tunaposti kila jambo mtandaoni, sio kila mtu ni lazima ajue mambo uliyoyafanya wikiendi.
- Kabla ya kufanya jambo jitahidi kuwaza kama hilo unalolifanya linaweza kutumika dhidi yako huko mbeleni. Skendo nyingi hasa za hivi karibuni zimekuwa za wanafunzi wa kike kusambaziwa picha za ngono na waliokuwa wapenzi wao.
Hili tunaweza kulisema kwa namna mbili, ya kwanza kwa upande wa wanaume wanaohusika, ya pili kwa upande wa wanawake wanaosambaziwa picha.
Mara nyingi chuoni ni sehemu ya kukua, vijana wengi wanakuwa bado hawajakua kujua dhamana na thamani ya mahusiano, wengi huwa wanakopi tabia na mambo ambayo wengine wanafanya.
Katika umri wa kwenda chuo wengi ndio wanaanza kujifunza au kufanya kwa uhuru zaidi mambo yanayohusiana na
96




























































































   94   95   96   97   98