Page 97 - Your Guide to University Life
P. 97

ngono, kama ni kuangalia picha na video za ngono, kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi nk.
Kwa vile sitaki kuonekana kama vile naelezea jinsi watu wanavyotakiwa kuishi kutokana na sheria zangu naomba ni waambie wanachuo wakiume kuwa unapokuwa kwenye mahusiano na binti wa watu, kuwa naye kama vile utakavyopenda mwanao wa kike afanyiwe utakapojaaliwa kumpata, lakini pia mambo ya nitumie picha au fanya hivi au vile ilinione unanipenda ni mambo ya kitoto sana ila pia fanya na ishi na watu kwenye mahusiano kiasi kwamba hata huko mbeleni ukiwa mtu mzima hauangalii maisha yako ya chuo kwa majuto kwa jinsi ulivyowafanyia wadada wa watu, kwa utoto mwanzoni inaweza kuonekana sifa, ila baada ya kukua unaweza jichukia kwa kumfanyia mwenzio ubaya ili upate sifa mbele za watu.
- Kwa wanachuo wa kike ningependa kusema kuwa jithamini, lakini pia usisite au kuogopa kuwa mkali linapokuja swala la mwili wako au unapoombwa kufanya vitu ambavyo haujisikii amani au hautaki kuvifanya. Usipende kupendwa sana na kukubalika na wanaume kiasi cha kuwa radhi kudharauliwa na jamii nzima au kujidharau mwenyewe.
- Punguza peer pressure, punguza kufanyia kazi mawazo ambayo sio yako, kila unapotaka kufanya kitu jiulize maswali magumu na jua kuwa umechagua wewe hayo maamuzi na utaishi na matokeo yake.
97






























































































   95   96   97   98   99