Page 95 - Your Guide to University Life
P. 95
Ufanye nini ukikutana na skendo chuoni?
Nahisi mwaka jana hii mada isingekuwa ya muhimu mimi kuiandika kwenye hiki kitabu, ila mwaka huu kumekuwa na uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi sana ya skendo haswa za picha za uchi na video za ngono kwa wanachuo.
Skendo chuoni ziko nyingi, nyingine huishia kujulikana chuo kimoja tu na nyingine husambaa kwa vile watu wanajua watu wengine na wanapenda kusimulia mambo ya watu kwa wengine hivyo unakuta imezidi kusambaa.
Na siku hizi hii mitandao ya kijamii ilivyo, jambo lolote linalotokea huku mtaani watu hupenda kuwa wa kwanza kwenda kulitangaza mitandaoni ili labda wapate umaarufu, kukuchafua au kupenda kuonekana wajuzi wa mambo.
Kabla sijaelezea mambo ya kufanya, ngoja nielezee jinsi ya kujiepusha na skendo;
- Ishi kwa kujua kuwa hakuna watu wapya duniani.
Hao unaokutana nao chuo, kuna mtu anamjua mtu, anayemjua mtu ambaye uliwahi kukutana naye vidato au shule au utakutana naye kazini. Vile unavyoishi hapo itasambaa, jitahidi kuishi katika namna ambayo ukiongelewa mahali hata kama itakuwa huko mbele kwenye maisha itakuwa ni kwa vitu chanya, watu huwa hawasahau hasa mabaya ya mtu na hayo ndio wanapenda kusimuliana.
Jitahidi pia kuishi kama mtu ambaye ikitokea ukabadilisha mambo unayojishughulisha nayo yale uliyokuwa unafanya
95