Page 93 - Your Guide to University Life
P. 93

Muonekano wako mbele za watu
Hapa napenda kuongelea vile unavyoji-present mbele ya watu. Najua huko nyuma vile unavyoji-present kwa watu haikuwa ishu kubwa sana, ila sasa hivi inabidi ujali kwasababu watu hawabadiliki, na vile watu wanavyokufahamu chuo huwa sio rahisi kusahau. Dunia hainaga watu wapya. Uliokutana nao shule utakutana nao kazini, uliokuwa nao primary umekutana nao chuoni, na uliosoma nao watafanya kazi na watu uliocheza nao, uliosoma nao primary watafanya kazi na uliosoma nao chuoni, yani dunia haina watu wapya. Image yako au vile unavyojipresent kwa watu itabakia vichwani mwao, watasahau kila kitu ila hawatosahau kwamba wewe ni muongo, ulikuwa mhuni, ulikuwa hiki ulikuwa kile.
Na unaweza kuta unataka kwenda kuomba kazi sehemu fulani lakini kwa vile dunia haina watu wapya huyu anamjua yule, na yule anajua ulikuwa mwizi chuo, na unakuta unakosa kazi. Unavyojulikana chuo au vile watu wanakuona inaenda mbali zaidi na hapo chuo inaendelea kwenye maisha na utu uzima wote, kwahiyo hapo inabidi uanze kujali na kubadilika. Kwa hiyo kuwa makini, ji-present vizuri kwa watu, jail muonekano wako, heshima yako. Lakini simaanishi uigize maisha au vile ulivyo mbele za watu, namaanisha ukue, uishi maisha kama mtu mzima mwenye wajibu wa maisha yake.
Kwa mfano kipindi mimi niko chuo, tulikuwa na hizo skendo na mnajua fulani kafanya hivi na vile, au yule ukikaa nae room moja ana roho mbaya au mchafu nk. Ukweli ni kuwa hivyo ndio vitu watavitangaza ukimaliza
 93






























































































   91   92   93   94   95