Page 91 - Your Guide to University Life
P. 91
- Uwe na sketi/ gauni / suruali / shati jeusi litakuokoa sehemu nyingi
- Ukiwa na shati jeupe pia litakusaidia, hivi unaweza vaa kwenye presentation, ukaenda nazo mtoko wa kiofisi kwenye usaili, au field au sehemu za kidini nk.
- Raba na sandals zitakufanya upendeze na chochote na pia ni rahisi kuzunguka nazo chuo
- Jeans, jeans, jeans
Nyeusi na bluu zinaweza kuvaliwa na shati za staili nyingi kwahiyo unaweza kuonekana tofauti kwa kubadilisha tu mashati.
- Saa au shanga ya mkononi au bangili inayoongezea urembo kwenye vazi ulilovaa
Kama ni mpenzi wa vitu vya nyongeza vya urembo basi ni vyema kuwa navyo, mimi nakuwaga na saa na bracelet yenye jina langu au bendera ya taifa. Ndio vitu ninavyovipenda, kuwa huru kuwa wewe, hiyo ndio maana ya staili yako.
- Ukivaa shati lenye rangi nyingi au vitu vitu vingi, vaa sketi / suruali/ kaptula yenye rangi moja. Labda rangi nyeusi au nyeupe au rangi mojawapo iliyopo kwenye rangi zilizopo kwenye shati.
91