Page 92 - Your Guide to University Life
P. 92

- Begi la mgongoni au begi lenye mkanda mmoja unaopita kifuani vitakufanya uonekane vizuri
- Chagua nguo wikiendi za kuvaa wiki ijayo ili usiwe unakurupuka kila siku
Ikija kwenye mitindo wengi huwa hatupendezi kwa kuwa hatukai chini kuchagua nguo, tunakurupuka asubuhi, kipindi saa moja tunawahi kwenda kipindi basi tunachukua tu shati linaloonekana haliitaji pasi ili tusichelewe.
Jiwekee tabia ya kuandaa nguo za wiki nzima wikiendi, ili usiwe unakurupuka bali unavaa kwa mpangilio. Kupendeza pia kunahitaji muda, muda wa kuchagua nguo unapoenda kununua, muda wa kujua staili yako ni ipi ambayo inakupendezaga, muda wa kupangilia nguo zinazoendana kwaajili ya kuzivaa.
Hayo machache ndio niliyojifunza kuhusu mitindo natumaini yatakuwa na msaada kwako pia chuoni. Lakini pia usiogope kujaribu mitindo tofauti na kujitofautisha vile unavyopenda, sijatoa ushauri huu ili nikubane, kuwa huru, mwili ni wako, unaruhusiwa kujaribu au kutengeneza staili ya mitindo inayokuwakilisha vizuri.
---
(Kujua nguo za kuvaa kwenye presentation ya assignment au ya project kwa wanaume na wanawake, bonyeza hapa)
 92



























































































   90   91   92   93   94