Page 94 - Your Guide to University Life
P. 94

chuo, hivyo ndio vitu vinavyokuja akilini nikisikia jina la fulani na fulani, na wao wakisikia jina langu. Unaweza kudhani kuwa ni muda mfupi tu na haina madhara na watu wachache tu ndio wanajua kuhusu hilo ila dunia nzima itajua kwasababu mtu anaweza kutolea mfano hata miaka na miaka ijayo kuhusu jambo moja tu ulilolifanya ambalo halikuwa na athari kwa wakati huo au wakati ulipolifanya ulihisi ni kwaajili ya umaarufu au ni trend kulifanya. Kwahiyo nikushauri uwajibike kwenye maisha yako, uwajibike kwenye maamuzi unayoyafanya ukiwa chuo, future yako inajengwa na wewe wa leo.
94

































































































   92   93   94   95   96