Page 108 - Your Guide to University Life
P. 108

-Kula vizuri na kwa wakati
-Kushiriki kwenye mambo ya kijamii na marafiki au kujitolea sehemu
-Tafuta msaada unapokuwa haujisikii hisia nzuri, kwa kuongea na rafiki yako, au mshauri wa chuo au dean.
-Jifunze kusema hapana kwa mambo mengine ambayo moyo wako unakataa kuyafanya. Kama ni kiongozi waachie wengine mambo ya kufanya. Kama unajisikia unahitaji kuongea na mtu kuhusu tatizo unalopitia unaweza ongea na mshauri wa wanafunzi, dean au hata ukatutumia DM Instagram (@maishayachuo) au WhatsApp – 0627975502.
-Jipende na ujithamini -Kunywa maji
-Kaa na watu wazuri, wanaokuhamasisha kufanya vitu chanya na wanaokujali.
-Andika hisia zako au ongea na mtu -Lia Kama unajisikia kulia
-Jiongelee maneno mazuri na chanya
-Punguza kupokea habari mbaya (kwa kufuatilia mitandaoni au kwenye maisha ya watu) au kukaa na watu wanaokufanya ujisikie vibaya
-Fanya sana vitu vinavyokuletea furaha
 108
























































































   106   107   108   109   110