Page 112 - Your Guide to University Life
P. 112

Mitandao ya kijamii, afya ya akili na masomo
Tunapenda sana kujua yanayoendelea duniani, mitandao ya kijamii inatusaidia kujua kila kitu na kwa haraka sana. Tunapenda kuonwa na watu na kuwaonyesha watu tuliyonayo au kuwa tuna furaha kwenye maisha yetu, mitandao ya kijamii inatusaidia kufanya hivi na kwa dunia ya sasa mitandao ya kijamii imekua ni majukwaa ya kukutanisha watu na kusambaza fursa hasa ukiitumia vizuri maana kazi za muda, mashindano mbalimbali hutangazwa huko.
Ila likija swala la masomo inabidi ujue jinsi ya kuwa na balance kati ya muda unaotumia mitandao ya kijamii na masomo yako. Nakumbuka tulivyokuwa chuo kwenye vikundi vya assignments na watu wako bize kwenye mitandao ya kijamii, hawachangii chochote, ila wanachati na kucheka tu, ilikuwa inaboa ila pia ilikuwa inatupotezea muda sana.
Kama upo mitandao ya kijamii na ni mtumiaji mzuri tu, naenda kushea njia chache zitakazokusaidia kujiwekea nidhamu ya matumizi ili u-balance masomo yako na muda wa mitandao ya kijamii kiasi kwamba haiathiri usomaji wako wala afya yako ya akili. Afya ya kili inakuja kwenye mitandao kwa sababu tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa matumizi ya muda mrefu ya mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha sonona, kujawa kwa habari kwenye ubongo (information overload) nk kwa vijana. Hivyo ni vizuri kuwa na matumizi yasiyoathiri maisha yako kwa namna ambayo ni hasi.
 112






























































































   110   111   112   113   114