Page 114 - Your Guide to University Life
P. 114

-Usiingie kwenye mtandao ukiwa kwenye lecture, tena nashauri uache simu room ukiwa unaenda kwenye lecture, sio tu unaonesha heshima kwa kufanya hivi, ila pia itakusaidia kuelewa na kuwepo darasani 100%.
-Usicheki mitandao ya kijamii ukiwa unadiscuss na wenzio. (Kuna mtu atakutaja kwenye kitabu atakachoandika kama mimi nilivyowataja classmates zangu, lakini pia ni vizuri kushiriki asilimia mia)
-Usicheki mitandao ya kijamii ukiwa unasoma, weka simu silent au iweke mbali. Muda mwingi tunaupoteza kwa kuangalia mitandao ya kijamii halafu unakuta masaa mawili yamepita na haujasoma kitu.
-Zima notifications, notifications ndio zinakufanya ucheki nani kaipenda picha yako mara masaa mawili yamepita na bado uko Facebook.
-Jiulize pia kwa nini upo? Je upo tu kwa vile kila mtu unayemjua yupo? Upo unapata kitu kwa kufuatilia hayo unayofuatilia? Au unatarajia kupata mkwanja kupitia mitandao hiyo kwa kutengeneza brand yako na kujitangaza? Kwanini haswa upo kwenye mitandao hiyo. Hii inakusaidia kufanya maamuzi yako bila kuwa yamehamasishwa na watu wengine bali ni maamuzi uliyokaa chini na kuyafikiria kuyafanya.
---
Siku hizi mitandao ya kijamii inawasaidia wengi kuingiza kipato kwa njia mbalimbali kama ni kitu unapenda kufanya pia basi ni vizuri kuanza biashara au kuwa influencer wa
114



























































































   112   113   114   115   116