Page 113 - Your Guide to University Life
P. 113

Njia zinazokusaidia kuwa na matumizi hayo ni; -Tenga muda wa kutembelea miitadao hii
Usiitembelee tu ukishika simu au ukiwa umeboreka, jiwekee muda na ukiisha unaendelea na mishe mpaka kesho tena
- Chukua mapumziko ya kijamii, kama una mitihani haina haja sana ya kucheki mitandao ya kijamii kwasababu sio notes, chukua mapumziko kipindi chote cha mitihani. Lakini pia mara nyingi huwa tunahisi tutapitwa, ila ukweli ni kuwa mitandao ya kijamii kuna mambo mengi hauwezi kuyamaliza yote hata kama ungetaka kuyajua lakini pia unapohangaika usipitwe kumbuka kuwa maisha yako mwenyewe yanakupita na unapoteza kwenye masomo.
-Angalia matumizi yako ya mitandao hiyo. Wengi huwa tunacheki tukiwa bored, na kama na wewe ni mmojawapo basi unatumia mitandao ya kijamii kukuondolea boredom. Kuna wengine tumekuwa mateja wa hii mitandao bila kujua, ni muhimu kuangalia ili ujue kama matumizi yako yamezidi hali ya kawaida. Kama umekuwa teja basi utakuwa unaitumia zaidi ya unavyotakiwa, jifunze kuji-control.
-Get a hobby. Tafuta kitu unachokipenda kufanya fanya, wakati wewe uko facebook toka saa tisa mpaka saa kumi na mbili, kuna mtu anacheza basketball, au anajifunza kupiga gitaa au ujuzi wowote ule anaoupata. Ni muhimu kujua kuwa kuna vitu vingine unavyoweza kuvifanya zaidi ya kufuatilia ubuyu wa mastaa au mpira. Tafuta vitu vingine pia vinavyosisimua ubongo wako uvifanye, hata shiriki mashindano basi zaidi tu ya kufuatilia ubuyu wa mitandao.
113





























































































   111   112   113   114   115