Page 125 - Your Guide to University Life
P. 125
Jinsi ya kula bata chuoni
Najua umesikia huu msemo ‘chuo bata’ mara nyingi sana, ingawa sio kweli kwa maana ya kwamba wewe utakuwa unakula bata tu muda wote, ila ukipanga ratiba zako vizuri unaweza kupata muda wa kula bata.
Chuo kigumu na unaweza hisi muda hautoshi kwa jinsi mambo na changamoto za ujana, fedha, kitaaluma, familia nk zinavyokusibu ila mbali na kuwa na yote hayo unaweza bado kula bata.
Kula bata / kupumzika / kuburudika ni muhimu kwasababu ni muhimu kupata muda wa kufikiria mambo mengine, ni muhimu kufanya mambo mengine pia zaidi ya akili yako kuwaza shule masaa 24, siku zote, kufanya hivi ni kuzuri kwa ajili ya afya yako ya akili pia na ya mwili.
Huu ni ushauri wangu mdogo kwako linapokuja swala la kula bata chuoni;
- Nakushauri kujua jambo unalopenda kulifanya kama starehe yako
Hii itakuondolea kufanya vitu ambavyo hautaki kuvifanya ila pia hautokuwa unafanya kwasababu ya presha ya marafiki.
- Jitambue
Kuna watu ambao wakianza tabia wanapotelea moja kwa moja, nina rafiki ambaye alipofika chuo akazama club na kunogewa ila baadae akaniambia anaacha kwasababu anaona anapotea kimasomo.
125