Page 126 - Your Guide to University Life
P. 126
Pia nilisikia stori ya rafiki wa rafiki yangu ambaye alinogewa na club kiasi kwamba akaamua kuacha chuo maana kinaboa, club kwake ndio ilikuwa inampa furaha. Jitambue.
Kumbuka kuwa unafanya hayo kwa kuwa wewe ni mwanachuo na una uhuru, ukikosa cheo chako cha uanachuo, maisha yanakuwa tofauti na hayo.
Jitambue na ujue mipaka yako likija kwenye swala la starehe.
- Kuwa na marafiki wanaokuambia ukweli
Marafiki wanakuzunguka wana matokeo chanya au hasi kwenye maisha yako lakini pia mnaathiriana. Hasa ukiwa chuo marafiki zako wanakuathiri sana, hivyo usiache kuwa na marafiki ambao pia wanakuambia ukweli unapokosea au unapojisahau.
- Kama unajua wewe ni mwepesi sana wa kuwa teja wa vitu kaa mbali na kujaribu madawa na pombe kali
- Hakikisha bata haliathiri masomo, hakikisha unakuwa na uwiano (balance), kila jambo ukilifanya kwa asilimia mia na pia kwa wakati wake. Muda wa bata kula bata vizuri tu, muda wa kusoma, kuwa makini na masomo.
126