Page 141 - Your Guide to University Life
P. 141
Kama unaona unahitaji nguvu sana kuelewa na unaona muda unakubana ni heri uache uongozi uweke nguvu kwenye masomo maana ukifeli chuo hauwezi tena kuwa kiongozi, wewe ni kiongozi wa dini chuoni kwa vile ni mwanachuo, ukiwa sio mwanachuo hauwezi kuwa kiongozi wa kikundi cha dini cha chuo.
Cha Kaisari mpe Kaisari kwa moyo wote, ishike elimu vizuri kwa vile umepata fursa ya kufika hatua hiyo. Wazazi hawatakuelewa ukifeli kisa ulikuwa kiongozi, kitu ambacho sio kilichokupeleka chuo.
141