Page 140 - Your Guide to University Life
P. 140
Kwanini viongozi wengi wa dini huwa wanafeli chuoni?
Hili ni jambo ambalo wengi huwa hatuliongelei ila huwa linatokea. Ni swali ambalo wengi wetu tunalo na kimya kimya tunajiuliza maana dini ni kitu ambacho ni nyeti kidogo kwahiyo kuongelea hadharani mambo kama haya labda inaweza ikaonekana ni kama kudhalilisha dini. Lakini ukweli ni kuwa hili jambo linatokeaga.
Inaweza kuwa muda mwingine dini inachukua muda mwingi wa maisha ya viongozi wa dini, kwahiyo unakuta wanashindwa kuwa na uwiano kati ya dini na masomo yao.
Nahisi sababu kuu ni hiyo, kwahiyo unakuta wanakosa kupumzika, wanakosa kuhudhulia masomo, wanakosa kupata muda labda wa kusoma na wengine nk. ‘Uongozi ni dhamana’ alisema hayati Magufuli, kwahiyo inaeleweka kuwa kazi inaweza kuwazidia kwenye eneo hilo la dini.
Nilipokuwa chuo nilikuwa naona viongozi wa dini wanavyochelewa kulala, muda mwingine hawali na hata kushindwa kuhudhulia lectures kwa vile majukumu ya dini ni mengi.
Imani ni nzuri, ila ni muhimu kujua kuwa unapokua chuo wewe ni mwanachuo unayesali sio mhubiri unayesoma. Ni muhimu kuwekeza nguvu kwenye masomo, cha Kaisari mpe Kaisari kwa moyo wote.
Ni muhimu kujua staili yako ya usomaji, kujua uelewa wako na kujua kumeneji mud a vizuri ili uwe unapata pia na muda wa kusoma.
140