Page 138 - Your Guide to University Life
P. 138
Vikundi vya dini chuoni ni vya muhimu kwa sababu mbalimbali;
1. Unapata ushirikiano na kikundi cha watu wanaokufahamu na kushirikiana na wewe katika yote.
Vingine vinakuwa vimefungwa sana kiasi kwamba unaweza usijihisi unaonekana au kama wewe ni sehemu ya hicho kikundi ila kwa wale waliozoeana unaweza pata hata marafiki wazuri wa muda mrefu kutoka kwenye vikundi hivyo.
2. Kuna kuwaga na safari ambazo haulipi gharama kubwa sana, mimi nimeenda safari nyingi na vikundi vya dini hata nilipokuwa sio mwanachama wa kikundi fulani kwa vile tu safari za wengi gharama hupungua, hasa mkiwa chuoni.
3. Mnapata nafasi ya kufanya wema kwenye jamii kwa pamoja na vikundi hivyo mfano michango kwaajili ya vituo vya watoto yatima nk
4. Dini na vikundi vya dini vinakusaidia kuwa mwangalifu hasa chuoni ambapo kuna mambo mengi ya kufanya kwa vijana, ukiwa na watu kama hao mnaosali/swali pamoja wanaweza kukusaidia kuendelea kushikilia mambo mazuri ambayo imani nyingi hufundisha kuyafanya.
Nakushauri kama mwanachuo huu ndio muda mzuri wa kujiuliza maswali ya dini ili uchague na uishike dini kama yako na sio kuishika na kuifuatilia kwasababu ya wazazi.
138