Page 137 - Your Guide to University Life
P. 137
Imani na maisha ya chuo
Nadhani watu wengi wanafuata mambo ya dini kwa urahisi wakiwa nyumbani kwasababu ya wazazi, lakini pia kwa shule za kidini hasa ukiwa kidato ni rahisi kuwa mfuatiliaji mzuri wa dini kuliko ukiwa chuo.
Uhuru wa chuo utakaokufanya wewe ufanye maamuzi yako mwenyewe kwenye maswala ya dini ndio unaonifanya niamini kuwa wengi walioshika dini wameshika kwasababu ya wazazi wao.
Kuna watu ambao wakifika chuo wanaendelea kuwa wafuatiliaji wazuri wa mambo ya dini, wengine wanasua sua, wengine wanaacha kabisa. Nahisi hizi hatua zote zina umuhimu, kwa vile uko mbali na wazazi unapata muda wa kujiuliza vitu vingi kuhusu mambo mbalimbali uliyokuwa unafanya ukiwa nyumbani, unajifunza na kujua mambo yapi ni yako na yapi ya kuyaacha kwa vile ulikuwa unafanya kwasababu ya mazingira. Dini ni jambo mojawapo ambalo ni la muhimu kuwa lako na sio la kulazimishwa na wazazi.
Kipindi hiki cha kujitegemea kinaweza kukufanya uendelee kufanya au uache kufanya yale uliyokuwa unafanya nyumbani lakini ni kipindi cha muhimu hasa kwenye ukuaji wa kijana. Chuoni kunaweza kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya maisha sio kwako tu hata kwa wengine uliosoma nao shule moja au unaowafahamu, kuwa muwazi kupokea na kushuhudia ukuaji na mabadiliko haya kwako na kwa wengine. Yawe tu chanya na sio yale yanayokuharibia maisha mfano kuwa teja wa madawa ya kulevya nk.
137