Page 135 - Your Guide to University Life
P. 135
kwasababu kadhaa zinazojulikana department ambazo wahadhiri waliziona za msingi.
Ukweli ni kuwa tulijitoa, lile si jambo la mchezo tulilolifanya kwa darasa zima kusimama na kutaka mabadiliko. Walimu hawatakiwi kututishia maishani ila kutusaidia kuelewa na kufaulu. Ni chuo tu ndio mwalimu anajivunia watu kufeli somo lake, ambalo ni jambo la ajabu sana. Sijui kwanini mwalimu anajisifia wanafunzi wanaofeli somo lake wanapokuwa wengi, kwasababu wengi wanapofeli inaonesha kwamba mwalimu hajui kufundisha na ndio maana wengi wamefeli, ila sijui wao kwa nini wanajisifia na kutishia wanafunzi, sio wote hufanya hivi lakini, ni wachache sana na unaweza hata usikutane nao.
Mgomo wetu ulikuwa mzuri haukutupa matokeo tuliyoyataka ila tulikuwa tumesikilizwa, tulikaa meza moja na wakuu wa department wakatueleza kwanini kumbadilisha ilishindikana nk. Ndio maana nashauri kama kuna njia nyingine za utatuzi na kusikilizwa, haina haja sana ya kuandamana kwa mabango maana njia ile hasa kukiwa na kiongozi mmoja tu mbele yeye ndio hupata matatizo mengi tofauti na wengine lakini pia kuna kuwa na usaliti mwingi ambao mkiungana kutafuta njia mbadala kwa pamoja hamtasalitiana sana kama wakiwa wachache mbele.
Zaidi ya hayo, migomo haswa ile inayosambaratisha amani huishia kuongeza muda wa kukaa chuo. Mara nyingi migomo kama hii ikifanyika chuo hufungwa kwa muda na wanafunzi huenda nyumbani, muda ambao unapotea.
135