Page 136 - Your Guide to University Life
P. 136
Kama kuna njia mbadala za kupeleka malalamishi, hizo ndio nzuri zaidi na kama hazifui dafu na lazima mgome, heri kugoma kwa njia tulivu, kama vile kugomea darasa badala ya kwenda mtaani. Shida nyingine ya kwenda mtaani ni kuwa mgomo unawezatokea kuwa na mtafaruku mkubwa na hata watu wakorofi wakaingilia na kutumia hali ile ya taharuki kufanya visanga kama kuiba na kuharibu mali. Ikifikia hapa, polisi huitwa na usipojiangalia, unaweza kujikuta unapigwa rungu au kupata mabomu ya machozi au hata kufungwa jela.
Ukijiunga na chuo pia ni vyema kuijua historia ya chuo, uelewe mambo yanavyoendeshwa. Unaweza kuwa na idea ya vile mambo yanafaa kuwa ukaona mnafaa mgome ili vitu vibadilishwe lakini kihistoria mambo yamekuwa hivyo hapo chuoni miaka na miaka, hata labda kuna waligoma kabla yako na bado mambo yakabaki hivyo hivyo. Si kwamba haufai kutaka na kuleta mabadiliko, lakini unafaa uelewe barabara na utumie your discretion.
136