Page 134 - Your Guide to University Life
P. 134
Migomo chuoni
Imetokea vyuo vingi, na umeshaisikia. Binafsi najua kuna watu ambao wamezaliwa kuwa wabadilisha mambo, na wako tayari kufa kwaajili ya ukweli wanaouamini na kuna wengine ni watazamaji tu na waongeaji wa yale ambayo wabadilisha mambo wanafanya. Nakumbuka nishashuhudia mgomo wa chuo kimoja nilipokuwa bado sekondari nahisi na niliona jinsi walivyofanyiwa baada ya kuandamana kiasi kwamba nimekuwa nawaza kama kwenye jamii zetu migomo inafanya kazi au kukaa meza moja ndio kunaleta suluhisho? Sijui.
Ila niseme tu naamini kuwa kila mmoja wetu ana nafasi ya kuleta mabadiliko sehemu aliyopo, kila mmoja wetu ana mchango chanya akisimama vizuri pale alipo, kwa jinsi nilivyoona sidhani kama migomo inakuwaga inaleta matokeo chanya labda kwa vile pia inategemeana na kitu walichokuwa wanaandamania. Kuna njia nyingi za kuleta mabadiliko ambazo pia ni muhimu kuzifikiria kabla ya kufika huko.
Nakumbuka tulipokuwa mwaka wa pili kulikuwa na mwalimu aliyekuwa anasema maneno ya vitisho kwetu kwamba tutafeli na wachache wetu ndio watakaofaulu nk, basi tukaamua kufanya mgomo ili abadilishwe. Haukuwa mgomo wa kwenda mtaani na mabango. Yule mwalimu alikuwa ni mwalimu wa department yetu, basi tukaenda department, tukasign form ya kumuondoa na kiaina tulikuwa tumegoma kufundishwa naye.
Wakuu wa department walikaa vikao na sisi, tuliongea ila mwisho wa siku hatukubadilishiwa mwalimu
134