Page 153 - Your Guide to University Life
P. 153

Unapomaliza chuo hasa kipindi ambacho unatafuta kazi au uko bize kuanzisha biashara au chochote kile kwaajili ya kujiajiri mara nyingi unakuwa hauna pesa unayoingiza.
Kwa hiyo unaweza kujikuta unaomba sio tu hela ya bahasha kwa ajili ya kuweka vyeti na CV unapoenda kupelekea vyeti sehemu uliyoomba kazi bali hata ya mafuta ya kupaka na nauli. Kuweka akiba kunaweza kukusaidia kuwa na hela fulani ya matumizi maana ukiwa ushazoea kupata hela halafu ikakata kuna kujisikia vibaya fulani kunatokea unapoomba kwa wazazi. Maana chuo ni kama ulikuwa unajitegemea halafu unarudi tena kuomba, inakusumbua hata wewe kidogo inaweza kuwa chanzo cha sonona unapokuwa na msongo wa mawazo kila saa kuhusu hela ya matumizi na majukumu ya nyumbani ambayo unatamani kushiriki kuyapunguza ila hauwezi.
Kwenye hili unaweza ukafungua fixed akaunti kama rafiki yangu mmoja alivyofanyaga na akaitumia hiyo hela kununua kiwanja au unaweza kuweka kwenye huduma za simu kama una nidhamu nzuri ya pesa na unaweza kushinda majaribu ya kutoitoa hata unapopitia hali tete unapokuwa chuoni.
Weka akiba pesa, hata kama ni kidogo, ndo ndo ndo si chururu, baada ya muda unavyozidi kuweka inakuwa kubwa lakini pia itakusaidia sana kuanzisha maisha mtaani hata kwa mwaka mmoja au kama ni kubwa hata miwili nk. Anza kuweka akiba toka ukiwa mwaka wa kwanza.
--Tumia kipaji chako, chuoni ndio mahali ambapo unaweza kujitafuta na kujijua upo na kitu gani ndani, tumia potential yako na uibadilishe kuwa chanzo cha kipato maana kuna
153





























































































   151   152   153   154   155