Page 151 - Your Guide to University Life
P. 151

Najua ukiwa chuo utataka tu kusoma na kula bata, na najua muda umebana ila kwa vile unaelekea utu uzima na kujitegemea ni lazima uanze kujiandaa na miaka yako baada ya chuo maana chuo ni miaka mitatu/minne/mitano nk lakini baada ya hapo una maisha yako yote huko mbeleni.
Hili ni zuri kwasababu una muda bado wa kujitafuta na kujua lipi la kufanya hata unapomaliza chuo na maisha yako yote, lakini pia hili ni baya maana kama hauna mawazo kabisa unaweza poteza muelekeo, unaweza pata sonona lakini pia unaweza shindwa kuweka bajeti nzuri kwa hela ambayo unaitumia tu kwa bata chuoni hasa kama umepata boom.
Unaweza kufanya maandalizi mbalimbali ya kuhusu maisha yako ya mtaani yatakuwaje unapokuwa chuo, maandalizi hayo ni kama;
--- Kujiuliza maswali magumu kama; Nisipopata ajira na hii kozi yangu itakuwaje?
Ni vizuri kuanza kufikiria swala kama hili mapema maana wengi hubaki tu kuamini kuwa wakiwamaliza chuo wataajiriwa lakini mara nyingi huwa haiwi hivyo ukija mtaani au haitokei kwa haraka kama unavyowaza itakavyotokea au pia inaweza kutokea ukaja kuwa haupendi ajira hiyo utakayoipata nk.
Ni muhimu kufikiria mambo haya yote mapema ili usiwe na msongo sana wa mawazo mwaka wa mwisho na pia ukifika mtaani baada ya kumaliza chuo.
151




























































































   149   150   151   152   153