Page 152 - Your Guide to University Life
P. 152
--- Kujifunza ujuzi wa vitu vingine au hata kujitolea sehemu mbalimbali ili vikuongezee sifa kwenye CV
Unaweza pata kazi kwa namna hii, unajitolea sehemu siku za weekendi au hata kuwa na mentor ambaye anafanya yale unayoyapenda ili ujifunze yale anayoyajua wakati bado uko chuo.
--- Kuanzisha lile jambo ulilokuwa unaliwazia kwa muda mrefu
Kama unapenda kuanzisha jambo fulani, iwe brand, YouTube, tovuti, au wazo lolote la biashara ambalo ungependa kuliendeleza au liwe chanzo chako cha fedha ukimaliza chuo, kuanza ukiwa chuoni kunakusaidia sana maana unakuwa umeanza mapema, una soko ambalo ni wanafunzi wenzio wako hapo chuoni lakini pia unapata ujuzi wa muda mrefu kuliko ukifika mtaani ndio kuanzisha jambo lako maana hapo utapoteza miaka kadhaa ya kujifunza na kuanzisha.
Kama utaanzisha biashara ni muhimu kujua kuwa unaweza ifikiria kwa mbali zaidi tu ya hapo ulipo chuo, inaweza kukuajiri ukimaliza chuo lakini pia wakati upo chuo wewe ni mwanafunzi mwenye biashara sio mfanyabiashara unayesoma. Jua lipi la kuliweka kwanza.
--- Kuweka akiba ya fedha ambayo itakuja kukusaidia hapo baadae ukimaliza chuo
Kama una boom, unaweza kuwa unaweka kiwango kidogo kidogo. Nakumbuka mimi nilipata boom na sio kwamba nilikuwa mla bata kivile ila tu natamani ningekuwa naweka akiba.
152