Page 4 - Your Guide to University Life
P. 4
Hongera!
Nakumbuka wakati nimemaliza kidato cha sita nilikuwa na wasiwasi wa matokeo yatakuaje. Yakatoka nimefaulu, nikawa na wasiwasi wa kupata chuo. Nilipopata chuo nikawa na wasiwasi wa maisha ya chuo yatakavyokuwa, nitautumiaje uhuru nitakaokuwa nao, masomo yatakuaje nk.
Najua na wewe uko sehemu hiyo hiyo, unajiuliza maswali mengi yanayozidi kukuogopesha kuhusu chuo na najua umeshasikia stori mbalimbali kuhusu maisha ya chuo ambazo pia hazijakutia moyo. Ndio maana nilipomaliza chuo niliamua kushea niliyoyapitia na wanaoenda/walioko chuo ili pia yawasaidie, na kuwaondoa woga na kuwapa dondoo zenye msaada kuhusu chuo.
Mambo, naitwa Eunice Tossy, mwanzilishi wa Maisha ya Chuo (Tovuti, YouTube & Instagram), jukwaa ambalo linashea dondoo kwa wanachuo ili kuwarahisishia maisha ya chuo na kutoa ushauri unaowasaidia kukabiliana na changamoto yoyote ile ambayo mwanachuo anawezaipitia. Maisha ya Chuo inawaunganisha wanachuo wote na waliomaliza katika kushirikishana mambo mbalimbali kuhusu chuo na maisha kwa ujumla, tunakurahishia maisha ya chuo ila pia tunakusaidia ujiandae na maisha baada ya chuo.
Kwanza kabisa ningependa nikupe pongezi, hongera sana kwa kufika chuo. Ni hatua kubwa. Tulipokuwa vidato lengo kubwa lilikuwa kufika chuo, na sasa umefika, umetimiza lengo, hongera sana ni hatua kubwa uliyoifikia.
4