Page 6 - Your Guide to University Life
P. 6

Tofauti 4 kati ya chuo na vidato 1 - Uhuru na Kujitegemea
Wote tunajua kuwa chuoni uko huru, unajipangia muda wa kusoma, unajipangia muda wa kula, unajipangia vile unataka kuishi maisha yako. Tofauti na vidato ambako kuna kengele, chuo una uhuru wa kutokwenda darasani na lecturer asikuulize.
Una uhuru, unajitegemea, unajiendesha mwenyewe kama mtu mzima. Wanakuamini sana kufanya maamuzi sahihi kwaajili ya maisha yako kwa vile wanajua umeshakuwa mtu mzima.
2 – Mashindano
‘Chuoni hakuna mashindano’
Unamjua aliyekuwa T.O kwenye matokeo yenu? Inawezekana unamjua, kipindi matokeo yetu yanatoka nilikuwa jeshini, tulikuwa na T.O pia kambi yetu, jamaa alikuwa wa tano kitaifa kama nakumbuka vizuri, tulikuwa jeshini ila taarifa zilisambaa tukawa tunamnyooshea vidole tu na kumuona kipanga balaa.
Madarasa yote ya nyuma kulikuwa na mashindano, nakumbuka shule ya msingi (nimesoma shule ya msingi ya Kinondoni) tulikuwa tunakusanywa madarasa yote A, B na C
   6



























































































   4   5   6   7   8