Page 8 - Your Guide to University Life
P. 8
yangu inawezekana wewe ushawahi tumia zaidi ya hela hizo hapo kabla.
Huku vidato hela haitumiki sana kuendesha maisha yako kama chuoni ilivyo, zamani ilikuwa ukilipa ada umemaliza ila chuo kama utakuwa haukai nyumbani basi utaanza kujitegemea kiuchumi, yani kupanga matumizi yako mwenyewe ya pesa. Hivyo unahitaji kujifunza matumizi mazuri ya pesa, kama ni kuweka bajeti ama kuwekeza kwenye biashara au kuweka akiba.
Ni muhimu kujifunza kuhusu pesa ukiwa chuoni, maana unahitaji huo ujuzi pia hata ukimaliza. Hivyo tumia muda wako ukiwa chuo kama majaribio na kujua/ kujifunza vizuri kuhusu mambo ya uchumi.
Jifunze kuweka bajeti ya matumizi yako, jifunze kuweka akiba ambayo inaweza kukusaidia hata muda ambao unaishiwa hela ya matumizi, jifunze kuhesabu mapato na matumizi yako ili usitumie tu hela bila mipango lakini pia kama unaweza na utakuwa na muda anzisha / wekeza kwenye kitu kinachokuzalishia pesa. Kikilipa vizuri hii hela inaweza kukusaidia hata ukimaliza chuo kujiendesha kimaisha.
4- Wahadhiri
Kwenye vidato mitihani ya mwisho ilikuwa inasahihishwa na NECTA, chuoni inasahihishwa na waliotunga, waliokufundisha, mhadhiri mwenye somo. Hii ni nzuri kwa
8