Page 7 - Your Guide to University Life
P. 7
ili waliotuongoza wapewe zawadi zao. Wanaitwa pale wanapewa chupa, vikombe nk. Ilikuwa inahamasisha kusoma, sana.
Ila pia inakuaminisha kuwa kuna mpambano, ni mashindano, na kila mtu anapigania kombe ambalo ni zawadi zinazotolewa.
Chuoni hakuna T.O, kuna watu watakaopata GPA ya tano, chuo chetu kilianza kutoa zawadi kipindi cha mahafali kwa vipanga hawa, na ni jambo zuri ila sio kwamba GPA yako inakufanya uwe mshindi darasani au uonekane umewazidi wengine. Na kwa vile ni siri yako, watu wengi huwa hawajali nani kapata nini.
Chuoni ni ushirikiano.
Maswala ya kuwa na notes ambazo mwalimu katoa na kuzificha ili usome wewe tu ili ufaulu ni ya vidato.
Mambo ya kujua mada fulani na kutowasaidia wengine ni mambo ya shule ya msingi.
Mambo ya kujifanya unajua wewe tu wengine wote hawaelewi kitu ni mambo ya sekondari, kwasababu semester hii unaweza ukaelewa sana, semester ijayo somo likakusumbua.
3 - Fedha
Kama utapata boom, na nakuombea upate maana litakusukuma kiuchumi, basi inawezekana ikawa ndio mara yako ya kwanza kupata hela kubwa kama hiyo kuitumia vile uonavyo, nasema hivyo kwa vile hiyo ndiyo ilikuwa hali
7