Page 5 - Your Guide to University Life
P. 5

Najua chuo utapewa prospectus na utakifahamu chuo ulichochaguliwa kwa undani na kozi yako, ila hiki kitabu kitakuwa kama muongozo wako wa maisha ya chuo mbali kabisa na kozi au sheria za chuo, ili usishtuke kwa changamoto utakazokutana nazo lakini pia kwasasa kikupunguzie woga maana kupitia hiki kitabu utajua hali halisi ya maisha ya chuo na jinsi ya kujiandaa kwenye maeneo mbalimbali kama vile kiuchumi, mahusiano, kitaaluma nk.
Kila mtu atapitia changamoto yake na inaweza kuwa tofauti na wengine, ila niko hapa kukuambia kuwa usiogope. Utasoma makosa niliyoyafanya chuo na yale mazuri niliyofanikiwa kuyafanya chuo ili uepuke makosa hayo lakini pia ufanikiwe mara mbili zaidi yangu. Natumaini kuwa kitabu hiki kitakupunguzia woga, kitakuandaa vizuri kwa maisha ya chuo na utahitimu huku ukiwa umekula bata na kufaulu masomo yako vizuri chuoni kama mimi nilivyofanya na zaidi ya mimi nilivyofanya.
Kama unahitaji msaada kwa mada ambazo hazipo kwenye kitabu hiki usisite kunitafuta :
Instagram - @maishayachuo
YouTube – Maisha ya Chuo (youtube.com/c/maishayachuo) Tovuti – maishayachuo.com
Email – admin@maishayachuo.com
WhatsApp/ Ujumbe / Piga - 0627975502
Eunice Tossy, Maisha ya Chuo
    5


























































































   3   4   5   6   7