Page 81 - Your Guide to University Life
P. 81
Njia rahisi pia inayoweza kukusaidia ku-move on kirahisi ni kujitahidi kufuta kumbukumbu zake. Watu wengi wanapoongelea ku-move on wanasemaga tafuta mpenzi mwingine, ila hii kiafya ya hisia na akili haiko vizuri sana kwasababu unakuwa haujamtoa mwingine, na unapeleka hasira na hisia ulizotoa kwa mwingine na kuzipeleka kwa mwingine mpya na unaweza kujikuta unaharibu mahusiano mapya kwa kuleta mambo na woga wa uliyopitia hapo kale.
Ni muhimu kuchukua muda kuachilia hisia zote ulizonazo kwa mahusiano na mpenzi aliyepita lakini pia ni muhimu kuchukua muda kujiuliza na kuona jinsi uhusiano uliotoka ulivyokubadilisha (self evaluation) ili usije ukaishi mabadiliko hayo (kama ni hasi) kwenye uhusiano mpya. Jipe muda wa kupona
Kila tunapoishi na watu tunajifunza vitu lakini pia wanatubadilisha kwa namna moja au nyingine, kama vile mtu anayependa kuangalia muvi za kikorea anajikuta kuna maneno au vitendo na yeye anavyovifanya alivovyiona kwenye muvi ndio sisi watu tunavyoathiriana kwa kuishi pamoja. Kwahiyo ni muhimu kujiangalia jinsi mahusiano yalivyokubadilisha (hasi au chanya) na vitu gani umejifunza kuhusu maisha na mapenzi kutoka katika uhusiano huo. Huku ndio ku-move on ninakokuongelea mimi.
- Kama mmeachana achaneni kwelikweli, kwenda mbele na kurudi nyuma ndio kunazidisha maumivu, yafikirie maumivu ya kufumua nyuzi na kushona upya kidonda.
Hii kurudiana na kuachana kunafanya unashindwa ku-move on. Ila pia unapofanya uamuzi amini kuwa moyo na
81