Page 80 - Your Guide to University Life
P. 80
Wengi tukiingia kwenye mahusiano tunajipoteza.
Tunasahau na kuacha kufanya vile vitu vilivyokuwa vinatufurahisha mwanzo, hili linatokea labda kwa vile kuna mwingine naye amekuja na vitu vyake anavyovipenda hivyo inabidi ujifunze vyake au pia inawezekana tu ni muda unakuwa haupo wa wewe kuwa bize na mambo yako, kwavile uko bize kuyaendeleza mahusiano.
Unapoachana na mpenzi ni muda wa kujitafuta, kurudisha furaha uliyonayo kwa kufanya yale ambayo yalikuwa yanakupa furaha ulipokuwa peke yako. Hii inakusaidia kuwa karibu na wewe uliyekuwa kabla ya mahusiano, na hivyo kumuachilia mpenzi moyoni kwa urahisi.
Lakini pia kwa kufanya hivi unajifunza kuwa na furaha na kujipa furaha mwenyewe.
Jitafute wewe ni nani bila ya hayo mahusiano. Mara nyingi huwa tunajitambulisha kwa kutumia wapenzi wetu bila kujijua sisi ni nani bila wao. Jitafute. Jichunguze, ujijue wewe, ili ukue kutokana na hilo ulilolipitia
- Lia
Kama unajisikia kulia, toa uchungu moyoni kwa kufanya hivyo. Kulia ni njia nzuri ya kuachilia hasira iliyopo moyoni au uchungu. Unapolia unakuwa mwepesi, na ndio hata kama wewe mwanaume unaweza na unaruhusiwa kulia pia.
- Futa picha, meseji au chochote kinachokukumbusha kuhusu yeye
80