Page 79 - Your Guide to University Life
P. 79

Jinsi ya ku-move on unapoachana na mpenzi wako
Mahusiano mengi ya chuo huwa hayadumu, yapo yanayodumu ila kwa ujuzi wangu na kusikia sehemu mbalibali hili jambo lina ukweli wake. Basi kwa vile inaweza kutokea ukaachana na mtu mkiwa chuo, hizi hapa ni mbinu za kudili na kuachana huko na ku- move on hasa kama ukiwa maeneo ya chuo;
- Jiandae kisaikolojia kumuona
Unaweza kumuona hata na mpenzi wake mwingine, jiandae kisaikolojia maana chuoni ni eneo ambalo mnaweza kukutana hasa kama mko kozi moja au mnashea lectures.
Unaweza kukaa naye mbali labda kwenye mawasiliano na kutoenda sehemu mlizokuwa mnakutana lakini kwa jinsi chuo kilivyo mnaweza kukutana kwa mengine, jiandae kwa hilo.
- Support system
Kuwa na marafiki, sio wote unaweza kuwaambia mambo yako ila kuwa na wale wa karibu unaoweza kuwashirikisha magumu unayoyapitia au vile unavyojisikia, hii inasaidia hata usipate sonona.
Lakini pia ukishiriki mambo ya kijamii na wengine inakusaidia kupunguza kujisikia upweke unaoweza kuwa nao unapoachana na mpenzi wako.
- Fanya vitu vinavyokufurahisha, kama ni kusikiliza muziki, kusoma vitabu, kufanya mazoezi nk
 79

























































































   77   78   79   80   81