Page 77 - Your Guide to University Life
P. 77
- Sio lazima upate mke/ mume chuoni
- Usiwe mke/ mume kwa mpenzi wako (girlfriend /
boyfriend)
- Unaweza kusema hapana sio kila anayekufuata una mjibu ndio kwa vile tu kakufuata na sio kila msichana unamfuata kwa vile tu ni msichana
- Jua kuwa mahusiano ni uwekezaji wa hisia, muda na wakati mwingine pesa. Mahusiano ya chuo huwa magumu hasa mkiachana wakati bado mnaonana, unaweza muona ex wako na mpenzi wake mpya inaweza kukuathiri hata kimasomo na maneno ya watu ndio usiseme, hivyo kama umeamua kuingia kwenye uhusiano chuoni jua gharama za uamuzi huo.
Mimi kama watu wengine niliumizwa mapema tu, miezi ya mwanzo kabisa ya kufika chuo kwasababu niliingia chuo na mawazo ya kwa kuwa niko huru ninaweza kutafuta mtu ambaye tutaoana, rafiki yangu wa kwanza kabisa wa kiume huyohuyo ndio nikajiwekea atakuwa mpenzi. Baada ya kuvunjwa moyo hapo nikajifunza, Usiwe na papara.
Sio lazima mwanaume wa kwanza au mwanamke wa kwanza kukutana naye awe wako, sio lazima upate mtu chuo, watu wanakutana popote pale maishani, huu sio mwisho. Kwa vile tu kila mtu yupo kwenye mahusiano haimaanishi na wewe ni lazima uingie kwenye mahusiano. Badala yake kua - jitambue, zurula, soma.
77