Page 75 - Your Guide to University Life
P. 75
Mahusiano
Ngoja niwe mkweli, wengi wanaoenda chuo wanafikiri ‘hatimaye sasa naweza kuingia kwenye mahusiano’, kwasababu tumezuiliwa sana huku nyuma, tunajua kwamba chuo kuna uhuru, kwahiyo upo huru hata kwenye maswala ya mahusiano. Ni kweli, ni jambo la ukweli. Na ndio maana kuna wapenzi wengi sana chuo, nani ana mahusiano na akina nani wameachana ni mada pendwa sana mazingira ya chuo, ubuyu.
Ila pia wengi wanaoenda chuo wanafikiria watapata mume au mke chuoni, wanahisi wakitoka bila mume/ mke basi kuna mahala walikosea au wamefeli.
Haya ndio mambo niliyojifunza kuhusu mahusiano ya chuoni:
1) Sio siri
Sijui watu wanajuaje ila mkishaonekana mara mbili pamoja wanahisi, na hata kama hamjawahi onekana wote, sijui watu wanajuaje aisee.
2) Mkiachana wakati mpo mazingira hayohayo, inaleta shida kidogo, wivu, kujisikia vibaya ndio unakuta watu wanajiingiza kwenye mahusiano mapya ambayo hawakupanga ili tu aonekane ame-move on na ameshamtoa yule mtu aliyekuwa naye moyoni.
3) Inaleta shida pia kama mpo darasa moja.
4) Mahusiano mengi ya chuo huwa hayadumu.
75