Page 73 - Your Guide to University Life
P. 73

-Kumbuka matukio yao muhimu. (Unaweza ukaweka siku zao muhimu kwenye kalenda ya Google na ikakukumbusha siku hizo zikifika. Ukiwatakia heri mapema, watahisi bado unawajali kwani umekumbuka bila kukumbushwa).
-Kwa marafiki zako walio off-campus, watembelee kipindi cha mapumziko wakati unasubiria pindi lingine, kula nao or kubalianeni uende kulala kwake (kama ni wa jinsia moja, hivyo usiku mnapiga stori). Ila hakikisha huyo unayeenda kwake kulala anapenda pia.
- Wikiendi zuruleni wote nk
- Kama umemkumbuka mtu fulani siku hiyo mtafute, itakupotezea mawazo ya masomo kwa muda mfupi ila pia utajikumbushia kumbukumbu nzuri kwa kuongea naye.
-Ukipigiwa kusaidia ishu fulani, saidia (ukipotezea tu, utaambiwa umebadilika toka ufike chuo, ila hakikisha kuwa una uwezo huo wa kusaidia, usiogope sana maneno ya watu kiasi kwamba ukafanya vitu ili tu kufurahisha watu wakati wewe unaumia).
Kama hauwezi tumia hekima katika kuwaambia au kufikiria suluhisho lingine, usijisikie vibaya, hauwezi kusuluhisha kila jambo, kila wakati.
-Tengenezeni group la chumba chenu, hivyo mtakuwa karibu wakati mnaishi pamoja na kufahamiana vizuri.
-Watembelee ndugu zako walio karibu na mji/mkoa au nchi uliyopo (watakusaidia kwenye mahafali). Lakini pia itakuwa nafasi yako ya kuwajua kwa undani hasa kama
73


























































































   71   72   73   74   75