Page 72 - Your Guide to University Life
P. 72
Jinsi ya kubalance kuwa na marafiki, masomo na mambo ya kijamii wakati muda na ratiba zinabana
Urafiki Masomo
Ni vigumu sana kuwa na uwiano (balance) chuoni kuna muda unahisi hata vitu ni vingi muda ni mchache au hata hauwezi kuviendesha vitu vyote ulivyonavyo au unavyotakiwa kufanya, ila ili kuepuka lawama za ndugu na marafiki watakaosema kwamba unaringa kisa umefika chuo na ndio maana hauwatafuti, inabidi ujue jinsi ya kuwa na uwiano na kutumia muda vizuri chuoni.
Hizi ndio njia chache za kuwa karibu na marafiki zako ingawa masomo na assignment zinakubana:
- Hakikisha unaongea nao, tumia muda unaoenda kununua chakula, kuwatumia ujumbe au kuwapigia.
72