Page 70 - Your Guide to University Life
P. 70

marafiki (kwamba inatokea tu uko nao) ila unafanya maamuzi ya kuchagua marafiki sahihi wa kuwa nao. Upweke usikuongoze kumruhusu kila mtu awe kwenye maisha yako.
Jinsi ya kupata marafiki (Dondoo za kutengeneza urafiki na watu wapya)
- Kuwa kimbelembele, anza kuongea na watu.
Usiogope anakuonaje kwasababu na yeye anawaza unamuonaje, kwahiyo kama kuna mtu unapenda awe rafiki yako/ au kuna kitu unahisi utajifunza kwake nk, vunja ukimya mfuate.
- Fanya uchunguzi, nasema wachuguze kwasababu hao watu watakuja kuwa na ushawishi/ kugusa maisha yako kihasi au chanya kwahivyo inabidi uwe makini sana nao, kama unaweza kuwachunguza kabla ya kuwaingiza kwenye maisha yako, itakuwa vizuri.
Kuna msemo unasema “nionyeshe watu watano kwenye maisha yako nitakuambia wewe ni mtu wa aina gani”. Unaweza tumia mitandao ya kijamii, watu wako wa karibu (ila isijulikane na usinitaje... kwaheri).
- Njia rahisi ya kupata rafiki mpya ni kushea vitu, anahitaji penseli mpatie.
- Watu wanapenda kuonekana kama maisha yao yanathamani, yanavutia kusikilizwa, hivyo wasikilize.
  70


























































































   68   69   70   71   72