Page 69 - Your Guide to University Life
P. 69

Urafiki na Mahusiano
Tuanze na urafiki;
Urafiki
Wanasemaga chuoni ndio sehemu unayoweza kupata marafiki wa maisha kwasababu utakuwa umekaa nao kwa muda mrefu ila pia ni mtu mzima kwa hiyo unauelewa mpana wa marafiki wa aina gani unawataka kwenye maisha yako. Lakini pia wanasema chuoni ndio sehemu peke ambayo utakuwa unazungukwa na marafiki zako kwa ukaribu kuliko kipindi chochote kwenye maisha yako.
Unawaza kwamba utawapata wapi hawa marafiki na chuo unachoenda haumjui mtu?
USIWAZE
Marafiki wapya unawapata kirahisi sana, kama vile wale,
- Utakao kuwa nao kozi moja.
- Utakaokutana nao sehemu ya usajili au ya chakula
- Utakao kaa nao chumba kimoja
- Sehemu za kidini
- Utakaokuwa nao kwenye michezo au hobbies zako
nyingine
Chuo kizima kimejaa watu ambao ukiamua watakuwa marafiki zako, chagua tu kwa hekima.
Siwezi kukupangia tabia za watu ambao inabidi uwe na urafiki nao, ila kwa vile unachagua hakikisha haupati tu
  69



















































































   67   68   69   70   71