Page 76 - Your Guide to University Life
P. 76

Huu ni ukweli, katika mahusiano yote niliyokuwa nayajua waliooana ni mmoja tu niliopata habari zao, wengine wote wameachana. Ikiwemo mimi pia na wote niliokuwa nao tulipokuwa chuo. Hivyo usiweke nguvu sana ukasahau masomo ambacho ndicho kimekupeleka wakati mahusiano yenyewe yana asilimia nyingi za kutokudumu.
Ila pia hata usipokutana na mtu chuo, maisha bado yanaendelea, mtakutana kwenye daladala, kazini, msibani, au atakuja kwenu kama mgeni nk kuna sehemu nyingi ambapo watu hukutana, usiwe na presha.
5) Mara nyingi yanatokana sana na msukumo wa marafiki (peer pressure)
Mahusiano ni mada kubwa sana ukiwa chuo, umri pia unachangia lakini kwa vile kila unapoenda unakuta watu wameshikana mikono au ukiwa chumbani unasikia mwenzio anaongea na simu wakati wewe unahangaika na kujisikia mpweke ni rahisi kuanza mahusiano kwasababu ya hii presha na sio mapenzi ya kweli kwa mtu.
Mambo ya kujua kabla haujaanzisha uhusiano chuoni;
- Kuwa na malengo, jua unachokifanya ili usipate hisia kwa mtu ambaye hana hisia na wewe
- Uliza, uongee na mtu ili ujue uhusiano wenu ukoje mapema kuliko kuwekeza wakati mwenzio ni mpweke tu hataki mahusiano
76



























































































   74   75   76   77   78