Page 84 - Your Guide to University Life
P. 84

Ushauri wa mambo ya mitindo
Wakati nafika chuo nilikuwa sijui kuvaa. Ni jambo la kawaida maana vidato vyote nilikuwa navaa sare ya shule ningejifunzia wapi mambo ya kujua kuchanganya rangi za nguo na staili za mitindo?
Basi bado nakumbuka nilivyokuwa navaa na hivi nilikuwa nimetoka jeshini yani bado nilikuwa kuruti, basi hadi kwenye kuvaa. Na hivi chuo kuna presha sana ya kupendeza na kuonekana wa maisha fulani ya tofauti (kuonekana kama una hadhi ya chuo nk), hivyo basi mbali tu na kuchekwa kwa vile nilikuwa nachanganya rangi zisizoeleweka ilikuwa rahisi sana watu kujua mimi mwaka wa kwanza. Ambayo siyo shida kwangu ila kwa vile ni binadamu tunayependa kukubalika ilikuwa inanisumbua kidogo.
Bahati nzuri madada niliokuwa nakaa nao hostel wa miaka ya mbele walikuwa wananielekeza kuvaa na kunisaidia kujua staili yangu, yani staili inayonipendeza mimi nikiivaa. Hawa walinisaidia pia jinsi ya kuchagua nguo na pia kuna rafiki yangu ambaye aliniambia mitindo ni kuwa simple, aliniambia nisivae mengi maana nilikuwa navaa koti, mtandio, cheni, vidude mkononi kibao, yani kila nilichonacho kabatini natembea nacho.
Sasa ili usipitie haya yote niliyoyapitia, ngoja nishee machache kuhusu mitindo yatakayokusaidia kutopitia mikasa yote niliyopitia mimi kwenye eneo la mitindo, nayo ni;
- Jaribu kujua staili unayoipenda na inayokupendeza 84
 




























































































   82   83   84   85   86