Page 85 - Your Guide to University Life
P. 85

Kuna staili nyingi sana siku hizi zinazotoka ila sio zote zinakupendeza unapovaa, hii inatokana na kuwa watu tuna maumbo tofauti na miili tofauti. Jaribu staili mbalimbali mpaka ujue ipi inakupendeza.
Ikija kwenye mitindo watu huwa katikati kwenye uchaguzi, ni labda uchague mtindo ulioingia / ulio maarufu kwa wakati huo au uvae mtindo ambao unaupendezesha mwili wako.
Ukivaa mtindo unaotamba, utapendeza kwasababu utaonekana umevaa staili iliyopo kwa muda huo, ukivaa inayokupendeza itaupendezesha mwili wako.
Nashauri kuvaa au kutafuta na kujua staili inayokupendeza kwasababu staili zinazotamba huwaga zinabadilika kila kukicha au baada ya msimu fulani kwa hiyo unaweza kujikuta unaingia gharama za kununua mitindo kila siku wakati ungejua nguo zinazokupendeza ingekuwa gharama rahisi na ungekuwa haupelekeshwi na mitandao ya kijamii na trends kwenye mavazi.
- Kuwa na nguo zile babu kubwa sio lazima zote ziwe za gharama
Najua hiyo point ya kwanza inaweza kukuumiza kama unapenda mitindo basi hii ikufariji kidogo. Unaweza kuwa na nguo zinazotamba ili uwe kwenye staili na wewe. Ukiwa nazo mbili tatu inakusaidia hasa kwenye mazingira kama ya chuo kuonekana hauko mbali sana.
85




























































































   83   84   85   86   87