Page 86 - Your Guide to University Life
P. 86

Huwa nashauri watu wengi hasa walioko chuo kujitofautisha, kujaribu kuvaa nguo kwa staili tofauti tofauti na kuwa wabunifu sio siku zote kuvaa sare chuo kizima mna staili moja, ila kama unaona peer pressure inaweza kukutesa maana unawezaonekana mshamba mbele ya kikundi cha marafiki zako basi kuwa nazo mbili tatu ili usiwe mbali.
- Kua na nguo za mitoko, na nguo za kushindia hostel, usichanganye
Kama unaendaga kanisani/msikitini/ sehemu yoyote ya dini unayoendaga, ni vizuri kuwa na nguo za huko na nguo za kushindia hostel au ulipopanga na nguo za kwendea lecture ambazo ni tofauti na za club nk. Hii inasaidia nguo zako pia zisifubae, lakini pia unaonekana una nguo tofauti kwa mazingira tofauti.
- Jaribu kujua nguo zinazoendana kutokana na rangi
Kama nilvyosema hapo mwanzo, swala la rangi lilikuwa tatizo moja wapo kwangu likija kwenye swala la mavazi. Sikujua kumbe kuna rangi zinazokupendeza, kuna rangi zinazoendana unapovaa juu mpaka chini na kuna rangi ambazo hautakiwi kuzivaa pamoja au kuzivaa mida fulani labda kwasababu ya hizo rangi zilivyo au kwasababu ya rangi ya ngozi yako. Wooh, mambo mengi kweli haya.
Lakini ni muhimu kuyajua, ni muhimu kujifunza kuhusu rangi ili ujue zipi zinaendana, zipi zinakupendeza unapozivaa (njia rahisi ya kujua hili ni pale unaposifiwa au
86




























































































   84   85   86   87   88